Tuesday, July 22, 2008

Kauli ya Kikwete

Inakatisha tamaa




Kulwa Karedia na Sauli Giliard


SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli ya kuwataka Watanzania kuvumilia kutokana na hali ngumu ya maisha, baadhi ya wananchi, wanasiasa na wasomi wamesema kauli hiyo imewakatisha tamaa.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti jana mjini Dar es Salaam, wananchi hao walisema hali hiyo imeonyesha wazi jinsi Rais Kikwete alivyoshindwa kuitawala nchi kwa kuwabebesha mzigo mzito walalahoi.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare, alisema Rais Kikwete ametoa kauli hiyo kwa nia ya kutafuta huruma kutoka kwa wananchi baada ya kuona uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 umekaribia.

“Rais ametoa kauli hiyo akiwa bado ana muda mfupi kukaribia uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, sisi tunasema kwamba ujanja huu hatuwezi kuuafiki” alisema Lwakatare.

Alisema umefika wakati sasa Watanzania kuelewa wazi kwamba nchi inakabiliwa na janga la kitaifa la kutokuwa na uongozi mzuri wa kushughulikia matatizo.

“Kama baba na mama ndani ya nyumba wanalia matatizo… je, watoto watafanya nini? alihoji kiongozi huyo huku akiwafananisha viongozi wa serikali kuwa ni sawa na wazazi, ambao hawatakiwi kulalamika mbele ya watoto.


No comments: