Karadzic akamatwa!
Radovan Karadzic, kiongozi wa zamani wa Waserb wa Bosnia, mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya halaiki aliyekuwa akitafutwa kwa uvumba na ubani na mataifa ya Ulaya Magharibi na Marekani, amekamatwa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Serbia (BIA).
Msemaji wa Rais wa Serbia, Bw. Boris Tadic, alisema Karadzic (Inatamkwa Karadzich) alikamatwa akiwa kwenye basi, kwenye kitongoji kimoja mjini Belgrade akiwa amefuga madevu. Karadzic amekuwa akiishi kwa kujifanya daktari za dawa za miti shamba. Bw. Karadzic anatuhumiwa kwa mauaji ya Wabosnia 7500 wa Srebrenica (inatamkwa Srebrenicha) mwaka 1995 kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Bosnia Harcegovina 1992 - 1995.

No comments:
Post a Comment