Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Lo lo lo lo lo, wiki hii kweli ni mimi ninayestahili lawama mpenzi. Sijui ilikuwaje maana nilikuandika bonge ya barua na nilivyojua, nikaituma. Nilikuja kushtuka sana uliponiambia kwamba hujaipata.
Ilibidi nimwombe Binti Bosi (BB) anisaidie, kumbe barua ilibaki kwenye ‘drafti’ sikuituma. Samahani sana mpenzi wangu. Sijui ilikuwaje.
Usifikiri hata siku moja nimekusahau maana nakuwaza kila wakati. Wewe ndiwe mwamba wangu. Ninapokasirikia kazi hapa, nakuwazia wewe na kutamani kupanda ungo nifike kwako mara moja. Ninapofurahia, nakuwazia wewe na kutamani kugawana furaha yangu na wewe. Nilalapo, niamkapo, nakuwazia wewe tu na hata siku moja siwezi kuacha kukuandikia.
Naomba radhi kabisa mpenzi usije ukanimwagia radhi maana hapo maisha yangu yatakuwa yamekwisha kabisa.
No comments:
Post a Comment