Na Hawa Mkombozi
Miss Universe Tanzania 2007, Flavian Matata ameula vikali baada ya kumwaga wino wa mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni kubwa ya uanamitindo ya Ice Model Agency ya Afrika Kusini ambapo aliahidi kwenda kufanya vizuri zaidi ya Magesse ambaye alikwishatangulia huko.
Flaviana alikwea pipa mnamo Juni 29, mwaka huu kuelekea Afrika Kusini tayari kufanya kazi na Kampuni hiyo inayojishughuliusha na maonyesho ya mavazi.
Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi alisema kwamba Flaviana amepata mkataba huo kutokana na umaarufu mkubwa wa Kimataifa katika mashindano ya Miss Universe mwaka jana alipoweza kutinga kumi bora.
Aidha, Maria alisema kuwa kampuni yake ilisimamia mkataba huo na mrembo huyo kuwa wa kwanza kupata nafasi hiyo kubwa hapa nchini.
“Hii ni mara ya kwanza kwa mrembo anayeshikilia taji la kimataifa hapa nchini kupata nafasi kama hii,” alieleza Maria ambaye alisimamia majadiliano na mkataba wa mrembo huyo.
Alisema mafanikio ya Flavian hayakuja kwasababu ya kwenda kuomba huko kwani mawakala hao wa Afrika Kusini hawajawahi kumuona zaidi ya kusikia habari zake na kuanza kumfuatilia mpaka kusaini naye mkataba.
Flaviana ni mlimbwende wa kwanza kuwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa kupitia urembo ya Miss Universe mwaka jana katika nchi ya Mexico na alifanikiwa kuingia kumi bora katika mashindano yaliyoshirikisha warembo 77 kutoka mataifa mbalimbali duniani
Chanzo cha habari Global Publishers Tanzania
No comments:
Post a Comment