Monday, July 14, 2008

Rostam apasua jipu



*Asema Tanzania inakabiliwa na wimbi la wivu, chuki
*Asisitiza kuwa safi, hahusiki na Richmond, Dowans
*Amwanika Mtikila kwa kumwomba, kupokea sh. milioni 3

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA inakabiliwa na kukithiri kwa wimbi la kuviziana, kutungiana uongo na kutakiana mabaya, imeelezwa.

Kauli hiyo nilitolewa jana na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz (pichani hapo juu), alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akifafanua kilichojitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kinondoni Julai 6 mwaka huu.

Siku hiyo, Bw. Aziz alikaribishwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la uzinduzi wa video ya kwaya ya Amkeni ya Kanisa hilo, ambapo pamoja na kuzungumza nao, alichangia sh. milioni 7.5 kwa ajili ya vifaa vya kwaya hiyo na jenereta.

Hata hivyo baada ya kufanya hayo, Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, aliitisha mkutano na waandishi wa habari akifuatana na wachungaji kadhaa wa Kanisa hilo na kumtuhumu Bw. Aziz kwa hatua yake hiyo.






1 comment:

Anonymous said...

Huyu jamaa katumia mbinu za hali ya juu za kutaka kujisafisha ufisadi kwa kutumia kanisa. Anajua kuwa kanisa ni chombo chenye nguvu nchini Tanzania....hivyo kama kanisa wakimsafisha, basi hata wengine tutamwonea huruma. Rais Mstahafu Benjamin Mkapa na Chenge walikosea waliporudi vijijini kwao kutaka kujisafisha...