Simu za mkononi
kusajiliwa kwa
vitambulisho!
SERIKALI imesema kuwa ipo katika mchakato wa kudhibiti matumizi holela ya simu za mkononi kwa kusajili namba za simu za watumiaji kwa kutumia vitambulisho vyao.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Maua Daftari ameliambia Bunge kuwa lengo la kufanya mpango huo ni kutaka kudhibiti matumizi mabaya ya simu za mkononi ambayo huhatarisha amani.
Akijibu swali bungeni lililoulizwa na Mbunge wa Bububu, Cosmas Masolwa (CCM), Dk. Daftari alisema mpango huo utahusisha kuboresha mfumo wa matumizi ya simu, hususani utaratibu wa sasa wa kuuza na kusambaza holela laini za simu.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali kupitia mamlaka yake ya mawasiliano iliunda kamati ya kitaifa inayojumuisha kampuni za simu, Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Mkurugenzi wa Mashtaka, TRA na idara mbalimbali za mawasiliano, yenye lengo la kuangalia njia ya kutunza majina na anuani za watumiaji wote wa simu za mkononi.
4 comments:
Haya mambo hayo Wabongo hatupitwi na kitu. Juzi juzi Waswidi walianza na ya kudaka TEKNOHAMA, Wabongo nao wameanza na kusajili simu za mkononi kwa vitambulisho!!!!!
Tusishangae na Wabongo. Wanorweji walianza na kusajili simu kwa vitambulisho kitambo kidogo. Ndivyo dunia inavyokwenda siku hizi...
Always I was wondering tutaendelea kuwa nyuma mpaka lini?? Ni aibu kuona serikali inashindwa kudhibiti hata jambo dogo kama matumizi holela ya simu za mikononi. Mheshimiwa daftari kuna mambo mengine hayaitaji kukuna vichwa sana wala kumaliza fedha za serikali. Itakuwa ajabu kama mpaka august serikali itakuwa bado haijafanyia utekelezaji wa suala hili. Hamuigi mfano wa huku India??
Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya taifa na kuwa na National Registry unaonekana. Ingekuwa rahisi sana kama kila Mtanzania angekuwa na kitambulisho cha uraia kufanikisha zoezi hili.
Wazo zuri lakini utekelezaji wake utakuwa mgumu. Kitambulisho cha kuonyesha tu wewe ni nani na unakaa wapi hivi vitatengenezwa mitaani vingi tu.
Post a Comment