Sunday, July 27, 2008

Suala la




Ni mgogoro wa

Katiba ya nchi



na Mwandishi Wetu

SASA ni dhahiri kuwa kuna mgogoro wa kikatiba nchini.

Hatua hii inatokana na msimamo uliotolewa juzi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ukipinga ule wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba Zanzibar si nchi, kama ambavyo inaelezwa katika Katiba ya Muungano.

Kwamba nchi imeingia katika mgogoro huo, ilithibitishwa na wanasheria kadhaa na watu wengine waliozungumza na gazeti hili jana na kuonya kuwa, suala hili sasa limefikia mahali pa kulazimisha uwepo mjadala mpana na wa wazi, kwa mustakabali mwema wa Tanzania.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, Mhadhiri katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alisema kitendo cha SMZ kutangaza msimamo unaokinzana na Serikali ya Muungano, ni sawa na kutangaza mgogoro wa kikatiba.

Akizungumza katika baraza la wawakilishi juzi, Naibu Waziri Kiongozi, Juma Ali Shamuhuna, bila kujali tamko la Katiba ya Muungano, alisisitiza kuwa Zanzibar ni nchi, na itaendelea kuwa nchi milele.


3 comments:

Anonymous said...

"ZANZIBAR SI NCHI au SI DOLA" ndio ilikuwa tafsiri ya kesi ya Duni Haji & Ors. v Republic. Katika kesi hii Mahakama ya Rufaa Tanzania ilisema kuwa Washukiwa hawawezi kutekeleza kosa la Uhaini katika sehemu ambayo sio Nchi (Zanzibar).

Katika kesi hiyo hiyo Dissenting Judgment ya Mheshimiwa Jaji Natalia Kimaro (Inayoenziwa na kuheshimiwa zaidi na Wanasheria TZ) ndio pekee iliyokubali kuwa ZANZIBAR NI NCHI kwa kuainisha vigezo ulivyovielezea katika waraka wako huu na kuzingatia vipengele vya Katiba. Lakini it was a Dissenting Judgment ! This is one of the Judgments which has distinctly raised Her Ladyship to the ranks of BOLD SPIRITS !

Ndio sababu Tume ya Jaji Kisanga ya mwaka 2000 ilipendekeza kuwe na Federation ya Serikali mbili. Kila nchi HURU; ya Zanzibar na ya Tanganyika ziingie katika Federation ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama unakaumbuka hili Mkapa alilikemea kupindukia hata kumsulubu hadharani Jaji Robert Kisanga kuwa amevuka mipaka ya Hadidu za Rejea (TORs) alizopewa na yeye (Rais) katika Tume yake!!!!

Na pia ndio sababu, Kipenzi chetu na Mwalimu wetu na Gwiji la Sheria za Katiba (Constitutional Law) Profesa Issa Gulamhussein Shivji hachoki kuandika makala, vitabu, na kutoa hoja kila siku kuwa Katiba ya Muungano (Articles of the Union): (a) Were not ratified properly and (b) were contravened & violated na kwamba Muungano huu ni wa Watu Wawili, wote marehemu marais wa nchi hizi mbili wa wakati huo.

Hivyo DONDA hili la Jamhuri ya Muungano would continue to fester and continue to produce pus which would eventually BURST to our detriment; na Utawala (executve) unajua sana hili isipokuwa kwa kuwa hali ilivyo iko kwa manufaa yao, hawataki jambo hili lizungumzwe, lihojiwe, liulizwe, na wala lijadiliwe ili lipatiwe muafaka.

MUNGU ATUNUSURU NA MISIBA TARAJIWA HII.

Anonymous said...

Waungwana,

Kuna vitu vinanishangaza kuhusu huu Muungano wetu kati ya Tanganyika na Zanzibar. Wakati sote tunakubali kuwa Muungano huu una kasoro nyingi, lakini walio juu hawataki au wanaonekana hawataki kasoro hizo zizungumzwe hadharani. Kila majadiliano yanapoibuka, yanaonekana kuzimwa haraka haraka ema na serikali ya Muungano au/na Chama cha Mapinduzi. Pana siri gani?

Halafu, inaonekana jina la Tanganyika ni kama vile marufuku kutajwa, Tanganyika inaitwa Tanzania Bara na Zanzibar inaendelea kuitwa Zanzibar na kuendelea kuwa na Rais wake, Bunge lake, Bendera yake na Wimbo wake wa Taifa.

Kauli ya majuzi ya Waziri Mkuu wa serikali ya Muungano, kuwa Zanzibar si nchi, imeleta zogo kubwa linaloendelea, hasa upande wa wenzetu wa Zanzibar. Inavyoelekea pamoja na jitihada zote zinazofanywa kuulinda na kuuimarisha muungano wetu huu, inakuwa vigumu kwa mtu kupata hisia kuwa Muungano huu umesimama imara.

Nafikiri, mpaka hivi niandikavyo hapa, kuwa Zanzibar ni nchi moja kati ya nchi mbili zilizomo ndani ya Muungano wenyewe. Hali kadhalika na Tanganyika bado ni nchi hiyo ya pili. Najua kuwa kikatiba Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni nchi moja. Lakini je, ni kweli ndani ya Jamhuri hiyo hamna nchi mbili zilizoungana?

Kama hamna na Zanzibar si nchi bali ni sehemu tu ya Tanzania. Je, inawezekana sehemu nyingine yoyote kuwa na Rais wake, Bunge lake (sheria zake), Bendera yake na Wimbo wake wa Taifa? Kama haiwezekani, kwa nini? Ikiwa sehemu moja ya nchi hii hii inaruhusiwa, kwa nini sehemu nyingine isiruhusiwe?

Mini nafikiri, tunaweza kufanya Jamhuri ya Tanzania, tukawa na nchi moja na serikali moja au tunaweza kuwa na Shirikisho la Tanzania, tukawa nchi mbili na serikali tatu. Hii Jamhuri ya MUUNGANO ya Tanzania yenye nchi moja na serikali mbili, haina ridhaa ya hawa wabia Tanganyika na Zanzibar. Ni hatari kuifumbia macho kasoro hii.

Anonymous said...

Karume asingeweza kutaka Muungano yeye, halafu aweke masharti yeye. Mwalimu ndiye aliyefuatwa na Wangereza kwa shinikizo la Marekani la kuzuia Wakomunisti wasipate uwanja wa kuweka Military base nchini Zanzibar.

Kimsingi hata Mwalimu alikuwa anataka kudhibiti usalama wa Tanganyika kwa kuidhibiti Zanzibar. Muungano huu tangu awali ulikuwa na manufaa zaidi ya kisiasa kwa Tanganyika ingawa pia Zanzibar imenufaika sana kiusalama pia. Vinginevyo Sultan Jamshid angekuwa kisharudi Bait-el-Ajaib.

Nafikiri matatizo ya Muungano ni ya kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Wakati Zanzibar inaingia kwenye Muungano ilikuwa haina tatizo lolote la kiuchumi.