Friday, November 07, 2008


Kula na kutapika ndio

mtindo wa kisasa


Kwa  Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,


Vibweka vya wakubwa Bwana!  Yaani!  Nimebaki kushangaashangaa hadi nasahau kufunga mdomo.  Kweli mpenzi.  Juzi nilimeza mbu watatu hivi hivi.

Hujambo lakini?  Wanimic ninavokumic?  Waniona katika bidhaa zako unazoziuza kama ambavyo mimi nakuona kwenye mashuka nikitandika, na kwenye masufuria ninapopika?  Mimi bado mzima kati ya wazimu, nakuwazia wewe tu.

Na vipi huko kwa binadamu?  Mnashangaashangaa kama sisi tunaokaa kwa miungu?  Mwizi Mungu aruhusiwa kurejesha.  Mwizi binadamdu apondwa na mawe.  Ama kweli ukubwa ni uhondo. 

Lakini labda hakuna haja ya kushangaashangaa.  Kwani wanene wanafanya tofauti na sisi?  Wale wezi wakubwa tunawaangalia na kuwashangilia hata sisi.  Tena wakitumwagia vijisenti vidogo vinavyotokana na wizi wao, au wakijenga kanisa au msikiti na pesa za wizi, au wakifadhili hili au lile, liwe mpango wa watoto yatima, liwe timu ya mpira sisi ndio wa kwanza kuwashangilia na kuwasifu … Lakini apatikane mtoto wa jirani anayeiba machungwa mawili kutokana na njaa kali, nani anamponda mawe na kumchoma moto.  Si sisi tu?  Mbona wengine hawachomwi?  ....bofya na endelea>>>>>


No comments: