Ubinafsi wa kupindukia
chimbuko la ufisadi
WENYE kuamini kuna Mungu na moto hujitahidi kujizuia kutenda maovu, na hata wakiyatenda, huenda misikitini na makanisani kutubu dhambi zao. Sijui ingekuwaje kama kusingekuwapo na wenye kuamini kuna Mungu na moto?Na nchi nayo ni hivyo hivyo, tukiamini kuwa kuna serikali ya watu, kuna mahakama huru, tume huru za chaguzi, kuna gereza, basi hata Waziri ataelewa kuwa asipoangalia, naye anaweza kuishia gerezani, kuishia motoni. Lakini, kama serikali ni ya kikundi cha watu, hakuna mahakama huru, hakuna tume huru za chaguzi, basi, magereza yatakuwa ni kwa walio nje ya kikundi hicho kinachoitwa Serikali na wenye kunufaika nayo. Jeuri na ufisadi wa baadhi ya viongozi hutokana na hali niliyoilezea hapo juu.
No comments:
Post a Comment