Sakata
Rais Kikwete apingwa
WATU waliotoa maoni kuhusu hotuba iliyotolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete, wamezipinga hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Waliliambia gazeti hili kuwa hatua hizo zilizochukuliwa na rais, zinamfanya aonekane amevunja Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa kitendo chake cha kuwasamehe watu walioiba na kurejesha fedha za EPA.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alisema Ibara ya 13 ya Katiba ya nchi inatamka usawa mbele ya sheria, hivyo kitendo cha rais kuwasamehe waliorejesha fedha hizo si sahihi na kusema inashangaza kwa nini rais anawakingia kifua watu hao.
“Rais Kikwete amekosea kutoa msamaha kwa hao mafisadi waliorejesha fedha hizo kwa sababu hao waliozirejesha wamekiri kosa na ushaidi wa wizi huo umepatika, kinachotakiwa, mafaili ya waliorejesha na ambao hawajarejesha yapelekwe kwa DPP ili awafungulie kesi mahakamani,” alisema Dk. Mvungi ambaye ni mwanasheria kitaaluma...bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment