Saturday, November 01, 2008

Sakata la vigogo waliochota mapesa kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), limechukua sura mpya, baada ya Idara ya Magereza nchini kuandaa vyumba maalum vya kuwaweka mafisadi hao ‘VIP ROOMS’ katika Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Habari za uhakika kutoka kwa vyanzo vyetu zinadai kuwa, vyumba hivyo tayari vimekamilika kwa ajili ya kuwaweka mafisadi hao.

“Vyumba hivyo vimetengenezwa katika mtindo wa chumba na sebule na ni mahususi kwa ajili ya watuhumiwa wa ufisadi wa EPA, ambao walishindwa kurejesha mamilioni ya pesa waliyoyachota isivyo halali hadi kufikia jana Oktoba 31, mwaka huu.

“Kila pati ina chumba na sebule, unajua wale ni watu wenye kuheshimika kijamii kwa hiyo wamefanyiwa hivyo ili kuendelea kuwaheshimu licha ya kwamba hawatakuwa huru kama mtaani,” kilisema chanzo kimoja.

Habari zaidi zinadai kwamba, vyumba hivyo vipo kwa idadi ya watuhumiwa wote kwa vile inajulikana licha ya kwamba haijafahamika ni wangapi watakuwa wamerejesha vitita hivyo mpaka tarehe ya mwisho aliyoiweka Rais Kikwete.  Bofya na endelea>>>>>


No comments: