Sunday, November 02, 2008


Sammy Korir,

Aeneza uvumi

Kuhusu Barack na

Michelle Obama.


……Ni kweli Obama

kazaliwa Marekani?

Ni Mkristo wa kweli?



Je, mnakumbuka sakata la Sammy Korir (pichani) kuwa alikuwa jasusi wa Polisi wa Norway?

Korir ameibuka tena na uvumi kuhusu Michelle Obama siku chache kabla ya uchaguzi wa Marekani. Korir anatumiwa na watu? Au ni kweli anavyodai kuhusu Michelle?

Michelle Obama amewahi kukanusha kuwaita Wazungu wa Marekani "Whitey" inadhaniwa kuna mkanda wa kuthibitisha kuwa Michelle alisema neno hilo hapo juu. Lakini mpaka leo, ushahidi huo wa kanda haujaonekana.

Sammy Korir anadai kuwa anao mkanda wa Michelle Obama kuwaita Wazungu "Whitey".


Korir anadai kuwa na makubaliano na Fox News ya kuwa wataurusha mkanda huo hewani. Fox News wamekana kuwa na makubaliano na Sammy Korir na African Press International. Korir anadai upande wa kampeni wa Obama unamtishia aliutoe mkanda huo kwenye vyombo vya habari na kuwa anapata msaada kutoka ubalozi wa Norway mjini Oslo. Msemaji wa ubalozi huo, Bi. Marit Andersen amekana hayo kwenye mtandao wa PoliticoKorir anadai mkanda alionao ni wa dakika 54

Madai ya Korir yamefika mbali na vyombo vya habari vya Marekani vimekuwa vikifuatilia madai hayo, vingine vimekuwa vikaandika kana kwamba madai ya Korir yana ukweli ndani yake (Right Pundits) na vingine vimekuwa vikiandika historia ya utapeli ya Korir (Mountain Sage - Sammy Korir, shady past, scams and hoaxes). Politico wameyapa madai ya Korir kichwa cha habari "Cover this! Inside the nastiest ´08 rumors."


No comments: