Friday, November 14, 2008

Siri mpya ya EPA

yaiumbua Kagoda


WAKATI watuhumiwa 20 wakiwa, hadi juzi, wamekwisha kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), ushahidi mpya umeibuliwa unaoonyesha kwamba kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, ambayo wahusika wake bado hawajashitakiwa, ilikuwa ya kwanza kuchota mapesa hayo zaidi ya miaka minane iliyopita.
 
Uchunguzi wa muda mrefu wa Raia Mwema umethibitisha kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ya kampuni ya Afritainer (T) Limited na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited ambayo hadi sasa wahusika wake na mahali ilipo ni kitendawili.
 
Kampuni ya Afritainer ilifanikiwa kuchota zaidi ya Shilingi bilioni 12 za EPA kwa kutumia nyaraka zilizosainiwa na watumishi wa kampuni moja maarufu ya Dar es Salaam (jina tunalo) wakidaiwa kuwa wakurugenzi wa kampuni hiyo kabla ya kufahamika kwamba hawakuwa wakurugenzi halali kisheria. 



No comments: