Friday, November 14, 2008


Iweje tuamke wakati

wanafanya juu chini kutupa

dawa za usingizi hadi

nusu kaputi?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,
Hapo vipi?  
Hapo si sawa!
Hapo chawa
Waota mabawa!


Ingawa chawa wengine angalao wameshindwa kuruka tena.  Eeeh!  Sijui wanaonaje kukaa huko!  Lakini bosi anachekesha.  Baada ya kuona nani amekamatwa, na yeye ameanza kutamba tena eti wasioweza kuEPA ni wengine tu.  Mwanasiasa msafi, au mtelezi hadi hashikiki.  Sanasana aweza kujiuzulu lakini ale umande wa rumande?  Thubutuuuuuuuu!!!

Na wewe ni mzima mpenzi?  Nakuhurumia na baridi yote hii na mvua.  Lakini usije ukavuta blanketi lisilo lako.  Au vipi? Vinginevyo nitakuEPA na mimi na hakuna cha rumande.  Au vipi? 

Bofya na endelea>>>>>


No comments: