Wajue marais 43
walioongoza Marekani
Rais wa Marekani ndiye mkuu wa serikali ya nchi hiyo. Urais wa Marekani ndio cheo kikubwa zaidi katika Taifa hilo, hasa ikizingatiwa kuwa Rais ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Marekani.
Kwa mujibu wa marekebisho ya 22 ya katiba ya Marekani yaliyofanyika 1951, hakuna mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa zaidi ya vipindi viwili mfululizo.
Kumekuwa na watu 42 walioapishwa kuwa Marais wa Marekani lakini—kwa upande mwingine—urais umetokea mara 43 kutokana na ukweli kwamba Grover Cleveland aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo mara mbili (1885–1889 na 1893–1897) kama rais wa 22 na wa 24.
Miongoni mwa wote waliochaguliwa kuwa marais, wanne walifariki dunia wakiwa madarakani kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “vifo vua kawaida”, mmoja alijiuzulu, na wanne waliuawa kwa sababu za kisiasa.
Rais wa kwanza alikuwa George Washington, aliyeapishwa mwaka 1789. Kwa upande mwingine, Rais aliyekaa madarakani kwa kipindi kifupi zaidi kuliko wengine wote ni William Henry Harrison. Akiwa Rais wa tisa wa Marekani na wa kwanza kufariki dunia akiwa madarakani, urais wake ulidumu kwa siku 32 tu. Aliapishwa
Machi 4, 1841 na kufariki dunia April 4, 1841.
Rais mwingine aliyevunja rekodi ya kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ni Franklin D. Roosevelt, na amejenga historia ya rais aliyekaa madarakani kwa vipindi vitatu mfululizo.
Rais wa kwanza wa Marekani, ambaye aliingia madarakani bila kupitia chama chochote cha siasa, alijulikana kama George Washington. Akishirikiana na makamu wake, John Adams, urais wake ulianza Alhamisi ya Aprili 30, 1789 na kumalizika Jumamosi ya Machi 4, 1797.
Hadi anaondoka madarakani alikuwa akiamini kuwa “Ni vyema kuwa mpweke kuliko kuwa na marafiki wabaya.”
Kuanzia Jumamosi ya Machi 4, 1797, Marekani ikampata Rais wake wa pili, John Adams, makamu wake akiwa Thomas Jefferson. Alikaa madarakani hadi Jumatano ya Machi 4, 1801. Hadi anafariki dunia Jumanne ya Julai 4, 1826, aliwasisitiza hivi Wamarekani wenzake: “Wajibu wetu kwa nchi hautakoma, ila maisha yetu ndiyo yatakayokoma.”
Alipoondoka madarakani Jumatano ya Machi 4, 1801, nafasi ya urais ikachukuliwa na Thomas Jefferson (1743–1826). Kama walivyo waliomtangulia, naye aliingia madarakani Machi 4, 1801 na kuondoka Machi 4, 1809. Alikuwa na makamu wawili ambao ni Aaron Burr na George Clinton. Kwa imani yake, “Mtu mwoga hukumbwa na ugomvi zaidi kuliko mtu shupavu.”
Rais wa nne aliitwa James Madison (1751–1836). Naye aliingia madarakani Machi 4, 1809 na kuondoka Machi 4, 1817. Makamu wake wa Rais walikuwa ni George Clinton na Elbridge Gerry. Madison aliwahi kukaririwa akisema: “Demokrasia si chochote bali utawala wa kundi la wenye fujo, ambamo asilia 51 ya watu hupokonya haki za asilimia 49 wengine.
Watano alikuwa James Monroe (1758–1831). Kama wale waliomtangulia, naye aliingia madarakani Machi 4, 1817 na kuondoka Machi 4, 1825.
Machi 4, 1825 akaja rais wa sita, John Quincy Adams. Utawala wake ulianza Machi 4, 1825 na kumalizika Machi 4, 1829. Adams alikuwa na falsafa iliyomuongoza. Alisema: “Ikiwa matendo yako huwatia moyo wengine na kuwafanya wawe na ndoto zaidi, wajifunze zaidi, na kuwa bora zaidi na zaidi, basi wewe ni kiongozi.”
Andrew Jackson (1767–1845), Machi 4, 1829, akachaguliwa kuwa rais wa saba. Kama walivyo waliomtangulia, aliondoka madarakani Machi 4, 1837.
Baada ya Jackson kuondoka, rais wa nane akawa Martin Van Buren (Democratic). Naye aliapishwa Machi 4, 1837. Kipindi chake kilimalizika Machi 4, 1841, makamu wake akiwa Richard Mentor Johnson.
Kisha akaja rais wa tisa, William Henry Harrison. Naye aliyeapishwa Machi 4, 1841 na kuondoka madarakani Aprili 4, 1841. Makamu wake wa rais alikuwa Whig John Tyler.
John Tyler akawa rais wa 10. Naye alichaguliwa Aprili 4, 1841 na kudumu madarakani hadi Machi 4, 1845. Rais wa 11 wa nchi hiyo akawa James K. Polk, ambaye naye alianza kazi Machi 4, 1845 na kuondoka Machi 4, 1849.
Marekani ilimchagua Zachary Taylor kuwa rais wake wa 12. Aliapishwa Machi 4, 1849. Utawala wake ulidumu hadi Julai 9, 1850. Makamu wake wa Rais alikuwa Millard Fillmore. Taylor alifariki akiwa madarakani Julai 9, 1850.
Rais wa 13, Millard Fillmore, ambaye aliapishwa Julai 9, 1850, utawala wake ulidumu hadi Machi 4, 1853 alipoapishwa Rais wa 14, Franklin Pierce, kuwa rais mpya wa nchi hiyo. Pierce naye alikaa madarakani hadi alipofariki dunia Machi 4, 1857, kutokana na kiharusi. Makamu wake akiwa ni William R. King.
Machi 4, 1857, James Buchanan aliapishwa kuwa Rais wa 15 hadi utawala wake ulipokoma Machi 4, 1861. Alikuwa akisaidiwa na John C. Breckinridge kama makamu wake wa rais.
Hatimaye Abraham Lincoln akachaguliwa kuwa Rais wa 16 wa Marekani na kuapishwa Machi 4, 1861. Aliendelea kuitumikia nafasi hiyo hadi alipouawa kwa risasi Aprili 15, 1865.
Andrew Johnson, ambaye alikuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa Lincoln, aliapishwa kuwa Rais wa Marekani Aprili 15, 1865. Alishikilia wadhifa huo hadi Machi 4, 1869 alipoukabidhi urais huo kwa Ulysses S. Grant.
Kisha akaja rais wa 19, Rutherford B. Hayes, ambaye aliapishwa Machi 4, 1877. Serikali yake aliiendesha akishirikiana na William A. Wheeler kama makamu wake hadi utawala wake ulipomalizika Machi 4, 1881.
Ndipo akaja Rais wa 20, James A. Garfield ambaye, kama wale wengine, aliapishwa Machi 4, 1881. Urais wake ulikoma Septemba 19, 1881 alipouawa
September 19, 1881 akaingia Rais wa 21, Chester A. Arthur mpaka alipomaliza kipindi chake Machi 4, 1885 na kukabidhi ofisi kwa Rais wa 22, Grover Cleveland ambaye naye alikaa madarakani hadi Machi 4, 1889.
Machi 4, 1889 akaapishwa Benjamin Harrison kuwa Rais wa 23 wa marekani mpaka pale alipolazimika kukabidhi ofisi kwa Rais wa 24, Grover Cleveland.
Rais wa 25, William McKinley, akaapishwa Machi 4, 1897. Alilitumikia taifa hilo hadi Septemba 14, 1901, na nafasi hiyo ikachukuliwa na Theodore Roosevelt kama Rais wa 26 wa nchi hiyo. alikaa madarakani hadi alipouawa Machi 4, 1909.
William Howard Taft, ambaye alikuwa Rais wa 27, aliapishwa Machi 4, 1909. Kipindi chake kilipomalizika Machi 4, 1913, ndipo alipokuja Woodrow Wilson, mwasisi wa Ushirika wa Mataifa. Aliapishwa Machi 4, 1913 na kuitumikia Marekani hadi alipoondoka madarakani Machi 4, 1921.
Kama walivyo waliomtangulia, Warren G. Harding, Rais wa 29, aliapishwa Machi 4, 1921. Kipindi chake kilimalizika Agosti 2, 1923, makamu wake akiwa Calvin Coolidge.
Ndipo Calvin Coolidge akaapishwa kuwa Rais wa 30 wa nchi hiyo hadi alipomaliza kipindi chake Machi 4, 1929, akisaidiana na Charles G. Dawes kama makamu wake.
Herbert Hoover, Rais wa 31, akaapishwa Machi 4, 1929. Alidumu madarakani hadi Machi 4, 1933, akisaidiana na Charles Curtis kama makamu wake.
Kisha yule rais aliyekaa madarakani kuliko wenfine wote, Franklin Roosevelt, akachaguliwa kuwa Rais wa 32 wa nchi hiyo. aliapishwa Machi 4, 1933. Alikaa madarakani hadi Aprili 12, 1945.
Aprili 12, 1945, Harry S. Truman akaapishwa kuwa Rais wa 33 wa nchi hiyo. Alidumu madarakani hadi Januari 20, 1953, ndipo akaja Rais wa 34, Dwight D. Eisenhower.
Januari 20, 1961, John F. Kennedy, Rais wa 35, akaapishwa kuliongoza taifa hilo. Hata hivyo, aliuawa kwa kupigwa risasi Ijumaa ya November 22, 1963. Nafasi yake ilichukuliwa na aliyekuwa makamu wake, Lyndon B. Johnson, ambaye alikuwa rais wa 36.
Ndipo akaja Richard Nixon kama rais wa 37. Aliapishwa Januari 20, 1969 hadi Agosti 9, 1974 alipolazimika kujiuzulu wadhifa wake wa urais.
Kutokana na kujiuzulu huko, Agosti 9, 1974, Gerald Ford aliapishwa kuwa rais wa 38 hadi Januari 20, 1977 alipokuja Jimmy Carter, rais wa 39. Alishikilia wadhifa huo hadi Januari 20, 1981 wakati Ronald Reagan alipoingia madarakani kama Rais wa 40, makamu wake George H. W. Bush.
Januari 20, 1989 George Bush aliapishwa kuwa Rais wa 41 hadi aliposhindwa na Bill Clinton katika uchaguzi wa Novemba 1992. Januari 20, 1993, Clinton aliapishwa kuwa Rais wa 42, akisaidiwa na Al Gore kama makamu wake wa Rais. Kipindi chake kilimalizika Januari 20, 2001.
Ndipo hatimaye akaja Rais wa 43, George W. Bush, ambaye aliapishwa Januari 20, 2001. inatarajiwa kuwa kipindi chake kitamalizika Januari 20, 2009, atakapoapishwa Rais wa 44, ambaye ni kati ya Barack Obama au John Macain.

No comments:
Post a Comment