Waziri wa mambo ya
ndani wa Iran afukuzwa
kazi kwa kuwa
na Ph.D batili
Bw. Ali Kordan
Waziri wa mambo ya ndani wa Iran, Bw. Ali Kordan amefukuzwa kazi na Bunge la nchi hiyo, baada ya kugundulika kuwa ana shahada batili ya juu ya falsafa (Ph.D) kutoka chuo kikuu cha Oxford. Cha ajabu zaidi, Bw. Kordan alikuwa akitoa mhadhara kwenye chuo kikuu cha Teheran huku akiwa hana hata shahada ya kwanza! Bw. Kordan alikuwa akiwahadithia wanafunzi wake, maisha yake akiwa Oxford, huku hata Oxford kwenye hajawahi kufika!
No comments:
Post a Comment