Aliyebadili jinsia
Afariki dunia
Afisa uhusiano wa Hospitali ya Muhimbili amethibitisha habari hizo kuwa Anti Aluu, amefariki dunia leo saa 1 na dk 05 asubuhi.
Kutoka kwa mdau anayemfahamu Dar es Salaam.
Habari LEO
Mkazi wa Dar es Salaam, Abdalla Aluu ‘Victoria’, aliyejibadili jinsi na kuwa mwanamke, amefariki dunia. Victoria aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kudaiwa kunywa sumu alifariki dunia jana asubuhi hospitalini hapo…
Majira
MGONJWA Victoria Armu aliyebadili jinsi amefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa baada ya kuhamishiwa akitokea Mwananyamala alikolazwa awali. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Muhimbili, Bw. Jezza Waziri, alisema hali ya marehemu ilianza kubadilika usiku wa kuamkia jana na kufariki saa moja asubuhi…bofya na soma zaidi>>>>>
Mtanzania
MWANAMUME aliyebadili jinsi na kuwa mwanamke, amefariki dunia. Mgonjwa huyo ambaye alikuwa gumzo kutokana na kubadili maumbile, alifariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amelazwa akiendelea na matibabu…bofya na soma zaidi>>>>>
No comments:
Post a Comment