Wednesday, May 27, 2009

Desmond Hatchett

miaka 29, ana watoto 20


Umeshawahi kumsikia Desmond Hatchett?

Amini usiamini, Desmond ana miaka 29 na ana watoto 20 na inasemekana ana watoto 21. Watoto hao amewazaa na wanawake 11 tofauti. Desmond ana matatizo ya kulipa gharama za kuwalea watoto, na ameliomba jimbo la Tennessee (Marekani) limsaidie. Jamaa anatakiwa awalipe mama za watoto kati ya Dala 25 hadi 305 kwa mwezi, na jamaa ana kazi inayompa mshahara wa kiwango cha chini. Kwa sasa jamaa anasota lupango kwa kushindwa kulipa gharama za kuwalea watoto wake


No comments: