Thursday, May 21, 2009

Dr. Harrison Mwakyembe, 

mbunge wa Kyela 

amepata ajali ya gari

 leo asubuhi.


Mwakyembe apata ajali mbaya Iringa 

Asubuhi Hii. Ajeruhiwa na Kukimbizwa Hospitalini.

Kutoka kwa mdau Haki Ngowi

2 comments:

Anonymous said...

Hii inadhirisha ukweli wa maneneo aliyosema dhidi ya mafisadi.Kwa nini aandamwe kila wakati kutaka kutoa roho ya kiongozi huyu shupavu?

Alitoka Kyela jana na inasemekana alipumzika Makambako jana usiku.Akadamka kuendela na safari yake Dar leo asubuhi. Baada ya muda kidogo dereva alianza kushindwa kuitawala gari barabarani na kisha ikagongana na lori. Inasemekana kulikuwa na watu wasiofahamika waliokuwa wakiifuata gari yake kutoka Kyela.Tairi la gari ya mbunge linasemekana lilichomoka katika ajali hiyo.

Wabongo mmeingiliwa, mko tayari kupambana na mafisadi? Mbunge huyu alijua hatari zote zilizopo kabla hajaanza vita hii.Kwa hulka yake hatishiki.Itakuwa aibu kama watanzania wengine watatishika baada ya tukio hili. Saa ya ukombozi imefika, mafanikio yapo jirani,vita si lelemama.

Anonymous said...

francisgodwin.blogspot.com anathibitisha baddhi yaliyozungumzwa katika comment hii.Lakini inasikitisha kwamba Francis Godwin ambae iaelekea, alikuwa Iringa wakati wa kuandika,hakumhoji dereva na alizungumza na wengine tu (wengine ambao hata majina hayajatajwa) kabla ya kuandika story yake.

Francis Godwin anasema ni matairi mawili ya mbele na si moja tu yaliochomoka- hali isiyo ya kawaida.Lakini Francis Godwin alishindwa kupiga picha ya gari sehemu ya matairi mawili ya mbele kutuonyesha jinsi yalivyochomoka.Kama yalichomokea sehemu za kufunga nati basi inawezekana ya yalilegezwa usiku pale Makambako maana gari ilisafiri vizuri tu kutoka Kyela mpaka Makambako.

Alafu Francis Godwin alishindwa kutupatia jina la hoteli aliyolala mbunge pale Makambako. Aidha ameshindwa kumhoji hata mtu mmoja kwenye hoteli hiyo.