Thursday, May 21, 2009

Vunja mbavu





Mama mmoja alikuwa akimuona mumewe kila siku kabla ya kwenda kazini anavuta bangi. Mama huyo aliamua kumuuliza mumewe:

“Mumewangu kila siku nakuona unavuta bangi, hivi ina raha gani?”

Mumewe alimjibu: “Hii inanipa nguvu ya kufanya kazi”.

Siku moja mama huyo aliamua kuvuta ile bangi ili naye apate nguvu, baada ya kuvuta, kwanza alianza kuchekacheka ovyo na baadae alimbeba mtoto wake kichwa chini miguu juu na kutoka naye nduki. Bahati nzuri akiwa anataka kutoka getini mumewe aliyesahau karatasi moja muhimu alimuona na kufanikiwa kumzuia kwani alifikiri alipatwa na ugonjwa wa akili.

Mume: Vipi mama Frank mbona umembeba hivyo mtoto na unakimbia naye?

Mke: Nimevuta bangi ndipo nimemchukua huyu kuku wangu nataka nikamchinje.

Aliposikia kauli hiyo ya mkewe, jamaa aliachana na bangi na kuamua kuokoka...

Kutoka Global Publishers (Tanzania)

No comments: