Saturday, May 23, 2009

Lo, kumbe kwa bosi kitovu ni

utovu wa nidhamu kabisa.



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

 

Mpenzi Frank,

Oo oo mpenzi nakupenda
Ee ee mpenzi nakutaka
Mpenzi eee
Mpenzi nakutaka 

Ungo mpenzi nimekosa
Nilitaka kujitosa
Ungo eee
Ungo nimekosa 

Bila wewe sina raha
Kila siku ninahaha
Wewe eeee
Wewe nakutaka 

Waninisikia mpenzi?   Nifanye nini wakati nakumic namna hii. Angalau mama bosi ameniongezea pesa kidogo kwa hiyo usishangae kunikuta nimekuja mara moja.  Na ole wako ninuse marashi ya mwingine wakati nafanya kazi usiku na mchana ili tuwe pamoja. 

Lakini usitegemee kwamba tutafunga ndoa ya dini.  Maana kwa kweli mpenzi naona dini ni duni sana upande wa sisi wanawake.  Eti kwa kuwa nyinyi wanaume ni wadhaifu lazima sisi tujifunike zaidi, tutoe jasho zaidi, tusivae tunavyopenda ili tusiwashawishi.  Eti nyinyi wanaume mkiona kipaja tu, au hata tako la nguvu ndani ya suruali mmekwisha!  Hivi ni kweli mpenzi nyinyi wanaume ni hopilesi kiasi hicho?...bofya na soma zaidi>>>>>

No comments: