Tuesday, May 26, 2009

Mgunduzi wa Viagra

afariki dunia


MWANASAYANSI kinara wa Marekani, ambaye alisaidia ugunduzi wa dawa ya kuongeza nguvu za kiume ya Viagra, amefariki dunia mjini Seattle, Marekani.

Robert Furchgott alitunukiwa Tuzo ya Nobel mwaka 1998 baada ya kugundua kuwa hewa ya nitric oxide ni muhimu katika kuongeza kuzibua njia ya damu mwilini.

Ugunduzi kuwa wa hewa hiyo kuwa inaweza kutanua mishipa ya damu ni moja ya maendeleo katika ugunduzi wa Viagra uliofanywa na kampuni ya dawa ya Pfizer.

Familia ya Furchott ilitangaza kuwa alifariki dunia jijini hapa Jumanne 19. Mei,  iliyopita akiwa na umri wa miaka 92.

1 comment:

Jamaldeen T.Bin Mazar E Shariff Ibn Zenjibari said...

Mwenyezi Mungu Amweke Pema. Amin