Alijipa mimba mwenyewe
akiwa jela
Mwingereza Samantha Orobator alikamatwa na gramu 680 za madawa ya kulevya aina ya heroine kwenye uwanja wa ndege wa Wattay nchini Laos na kutupwa gerezani akikabiliwa na adhabu ya kifo.
Kwa mujibu wa sheria za Laos, mtu anayepatikana na madawa ya kulevya yenye uzito zaidi ya gramu 500, adhabu yake ni kuuliwa kwa kupigwa risasi.
Samantha Orobator aligundulika kuwa na mimba ya miezi mitano ambayo aliipata akiwa tayari gerezani kwani alikuwa jela tangia mwezi wa nane mwaka jana.
Taarifa zilisema kwamba Samantha inasemekana alipitishiwa barua kutoka nje ya jela na barua hiyo ilikuwa na sindano iliyokuwa imejazwa mbegu za kiume.
Mamlaka za Laos zimeshikilia madai hayo ya Samantha kujipa mimba mwenyewe kwa kutumia sindano kwakuwa walikuta sindano kwenye chumba chake cha jela.
Samantha inasemekana alijipa ujauzito ili kukwepa adhabu ya kifo kwakuwa wanawake wajawazito adhabu zao za kifo hugeuzwa vifungo vya muda mrefu jela.
Mwanzoni kulikuwa na tetesi kwamba mwanaume wa Kiingereza ambaye naye alifungwa katika jela hiyo ndiye aliyempa ujauzito huo Samantha lakini Muingereza huyo alikanusha vikali tetesi hizo akisema kwamba ni vigumu sana kwa yeye kuwa na uhusiano na Samantha kwakuwa wametanganishwa na fensi.
Serikali ya Laos iliiahirisha kesi ya Samantha kwa muda ikijaribu kujua undani hasa wa jinsi Samantha alivyopata mimba.
No comments:
Post a Comment