Wednesday, May 13, 2009

Wakosa uraia kwa kudanganya

walipokuja Norway.


Mohammad toka Afghanistan 
"Nilidanganya nilipokuja Norway, sasa najuta"


Mohammad kutoka Afghanistan ni mmoja wa wageni 8500 waliokataliwa uraia kwa kudanganya na kutoa sababu za uongo walipokuja Norway kuomba hifadhi za kikimbizi, linaandika gazeti la kila siku la Aftenposten la leo.

Mohammad ameliambia gazeti la Aftenposten kuwa amedanganya kusema njia aliyotumia kutoka Afghanistan hadi kufika Norway. Ukweli ni kuwa alipitia Finland na alipohojiwa na polisi wa Finland alisema jina lake. ”Abdul” .

Mohammad ambaye alikuwa rubani wa ndege za kivita za aina ya MiG-21 kwenye jeshi la anga la Afghanistan, alikuja Norway kupitia Urusi na Sweden kabla ya kuja Norway. Mohammad alipata kibali cha hifadhi ya kikimbizi kwa ”sababu za kibinadamu”. Baada ya miaka miwili toka kuja Norway, mkewe na watoto wake waliruhusiwa kuingia Norway kwa sababu za baba yao.

Mohammad amegundulika kuwa alidanganya kiasi flani. Ameomba uraia yeye na familia yake, lakini wamekataliwa kwa sababu za kudanganya alipokuja kuomba hifadhi ya kikimbizi. Kinachomsikitisha ni kuwa mtoto wake wa mwisho ambaye amezaliwa hapa Norway, naye kanyimwa urai kwa kosa alilofanya baba yake.

Wengi wanaokataliwa uraia kwa sababu kama za Mohammad wanatoka Afghanistan, Irak na Somalia. Asilimia 96,5 ya wote wanaokuja kuomba hifadhi za kikimbizi hapa Norway hawana vitambulisho vya aina yeyote ile vya kuthibitisha walikotoka, hivyo inakuwa vigumu kwa idara ya uhamiaji na polisi kuwaondoa nchini, idara ya uhamiaji (UDI) imeiambia gazeti la Aftenposten.

No comments: