Akamatwa kwa kujisifia kwa
Mtu mmoja Saudi Arabia amekamatwa nchini Saudi Arabia, kwa kuzungumzia na kujisifia kuhusu maisha yake ya ngono kwenye luninga. Mazen Abdul Jawad alizungumza hayo wiki iliyopita kwenye kwenye stesheni moja ya TV nchini Lebanon, LBC. Inaripoti Arab News toleo la Kiingereza.
Kipande cha sehemu ya mazungumzo yake "Red Line" kiko kwenye You Tube na jamaa (miaka 32) anazungumzia kwa kinaga ubaga jinsi anavyofanya ngono.
Kutokana na kanuni na sheria za Saudi Arabia, si wanaume au wanawake wanaruhusiwa kufanya ngono kabla ya ndoa. Na mtu akikamatwa na polisi wa maadili nchini humo adhabu yake ni viboko mbele ya kadamnasi ya watu au hata adhabu kali inaweza kutolewa.
No comments:
Post a Comment