Norway iache kutoa misaada
Hela za misaada ndizo zinazoongeza ufisadi nchini Tanzania, Tone Ellefsrud ameliambia gazeti la kila siku hapa Norway (toleo la Jumapili ukurasa wa 12 na 13). Bi. Ellefsrud amefanya kazi miaka saba nchini Tanzania. Tone amekuwa kwa akijitolea bila malipo kwenye hospitali moja mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
Tone anasema kasheshe ilianzia bandarini Dar es Salaam na Tanga. Tone alikusanya hela kwa nguvu zake mwenyewe, akanunua vifaa vya hospitali ambavyo alivitia kwenye makonteina matatu. Alipoenda kuchukua hayo makonteina, aliwaambiwa ayalipie Dala 200,- kila konteina. Na kila siku iliyokuwa ikienda bila kuyakomboa hayo makonteina bandarini alikuwa anatozwa faini.
Tone Ellefsrud aliamua kuacha kazi aliyokuwa anafanya ya nesi msaidizi kwenye hospitali ya mkoa wa Buskerud, Norway na kwenye Chama Cha Msalaba Mwekundu. Pia alikuwa naibu kiongozi wa chama cha Labour, mkoa wa Buskerud ana kwenye shughuli zake za kisiasa alipigania sana kuongezwa kwa misaada nchini Tanzania. Lakini toka ameishi Tanzania, amebadili mwelekeo wake huo wa kuhusu misaada.
Tone anasema kuwa Norway iache kutoa misaada kwa Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili, ili kuifanya Tanzania ifikirie na ibuni yenyewe mbinu za kuongeza kipato cha taifa badala ya kutegemea misaada.
Anaendelea kwa kusema kuwa alipofika Marangu, hospitali ya hapo haikuwa na kichanganua vipimo vya damu. Akahangaika kutafuta hela yenyewe mwenyewe kwa wafadhili nchini Norway, na akakinunua kwa kroner milioni moja.
Mwaka 2006 mkuu wa maabara wa hospitali hiyo akapotea mitini na kifaa hicho. Inasemekana jamaa huyo anaendesha hospitali yake binafsi mjini Arusha. Jamaa alikamatwa na kushtakiwa, lakini hakufungwa kwa vile anajuana na watu.
Bi. Tone Ellefsrud anaendelea kusema kuwa sehemu kubwa ya misaada kwa Tanzania inapitia makanisani na huko anasema kuna uozo wa hali ya juu. Hela zinapotea huko hazijulikani zinakoenda. Wakati mwingine mambo yanayofanyika makanisani hayaendani kabisa na kanuni na maadili ya kanisa, amesisitiza Bi. Ellefsrud.
Askofu wa dayosisi ya Kaskazini, Martin Shayo alipopigiwa simu na gazeti la Aftenposten kujibu tuhuma za Bi. Tone Ellefsrud, aliyapinga vikali madai hayo. Bi. Tone, amelionyesha gazeti la Aftenposten risiti, vielelzo na picha za shughuli nyingi alizolipia kuwa hazikufanyika, hela zimeliwa na wafanyakazi wa kanisa.
Mwaka jana Bi. Tone alipotishia kulishtaki kanisa kwa ubadhirifu wa hela, kanisa lilimfukuza asifanye tena kazi hospitalini. Pia walimfukuza nyumba waliyompa aliyokuwa anakaa. Waliharibu gari lake na waliwahi hata kumtishia maisha yake. Bibi wa watu akakimbilia Rwanda kwa rafiki yake.
Bi. Tone Ellefsrud amerudi tena Marangu. Anajishughulisha na shughuli zingine. Anasema kwa hategemei kurudi na kuishi Norway.
Chanzo cha habari ni gazeti la Aftenposten la leo Jumapili 26.7.2009 (ukurasa 12 na 13)
No comments:
Post a Comment