Thursday, July 30, 2009

Amwagia mumewe maji

ya moto kwenye nanihii

baada ya kuchoshwa na

uzinzi wake…..



Afanya kama alivyofanya Lorena Bobbitt , mnakumbuka?


Emmanuel "Ojo" Ojofeitimi.


Mwanamke mmoja nesi mwenye miaka 67, Bi. Oyinda Ojofeitimi wa Milburn St. in Springfield Gardens, New York, amemwagia mumewe maji ya moto kwenye nanihii yake, baada ya kuchoshwa na tabia za uasherati za mumewe, Bw. Emmanuel “Ojo” Ojofeitimi (ambaye pia ni nesi, miaka 67). Bi. Oyinda alifanya kitendo hicho saa 12 za asubuhi juzi, wakati mumewe akiwa usingizini. Emmanuel aliamka na kulia kwa maumivu makali, akiweweseka bila kujua nini kimemsibu!

Bi. Oyinda alipiga mwenyewe simu na kuwataarifu polisi. Amewaambia polisi kuwa ni hivi karibuni amegundua tabia za uzinzi za mumwewe za miaka 20!!! Bi. Oyinda yuko nje kwa dhamana ya Dala 100 000 za Kimarekani (laki moja)

Mumewe amelazwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Nassau. Bi. Oyanda ana asili ya visiwa vya Grenada, wakati “Ojo” ana asili ya Naijeria.

Vyanzo vya habari: New Yorks Daily News na New York Post.


No comments: