Wednesday, July 22, 2009

Dalia Mogahed,

Mshauri wa Rais Obama:

Masuala ya Waislam nchini

Marekani.Anavaa hijabu!



Dalia Mogahed, mshauri wa Rais Obama kuhusu masuala yanayowahusu Waislamu nchini Marekani.


Dalia Mogahed ni mchanganuzi mwandamizi (senior analyst) na mkurugenzi mkuu wa Gallup Center for Muslim Studies nchini Marekani alichaguliwa na Rais Obama mwezi Aprili mwaka huu kuwa mshauri wake wa masuala yanayowahusu Waislamu nchini Marekani.

Wazazi wa Dalia walihamia Marekani takriban miaka thelathini iliyopita, akiwa na miaka mitano. Hivi karibuni akiashirikina na Profesa wa sayansi jamii, John Esposito wameandika kitabu kinachoitwa “Who Speaks for Islam?”

Mogahed alipata shahada yake ya kwanza ya uhandisi kemia na shahada ya uzamili ya MBA kutoka chuo kikuu cha Pittsburg. Mogahed anaishi Washington D.C. na mumewe na watoto wao wawili wa kiume.


Bofya na soma mahojiano na Mohammed Al Shafey wa Asharg Alawsat


Msikilize Dalia Mogahed na Dr. John Esposito wakihojiwa na Riz Khan wa Al Jazeera





No comments: