Tahadhari toka kwa
Tafadhali wajulishe wote wanaohusika kwamba kuna kundi kubwa la majambazi wenye silaha kali, ambao wameingia Jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wahalifu hao ni pamoja na Wakenya ambao wana tabia ya kupora fedha katika taasisi kubwa kama, mabenk, kampuni za mafuta na sehemu zenye biashara kubwa n.k .
Aidha watu hawa wana mbinu ya kula njama na watumishi wasiokuwa waaminifu. Ni muhimu mkafuatilia mienendo mbalimbali katika benk zenu na sehemu zilizotajwa hapo juu pamoja na kuimarisha usalama julisheni kwa message kupitia namba
0783034224
au kwa simu ya mdomo
0754-034224
0787034224
zote ni namba za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam.
Namba zingine za simu ni
0754- 276217
0776880000
namba hizi ni za mkuu wa Upelelezi Kanda maalum.
Lengo la maelezo si vitisho kwenu bali ni tahadhari muhimu , inayofaa kuzingatiwa,
S. H. Kova - SACP
KAMANDA WA KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment