Jana mtoto mmoja ameshikwa na mafua ya nguruwe kwenye Norway Cup. Hali yake si mbaya sana. Daktari wa Norway Cup, Dag Arne Daljord amesema kuwa idadi ya watoto watakaoshikwa na mafua ya nguruwe kwenye mashindano hayo, ikifikia 50, basi kuna uwezekano yakasimamishwa.
Hadi hivi sasa watu walioambukizwa na mafua ya nguruwe nchini Norway, wamefikia 245, imethibitishwa na idara ya afya ya Norway. Wiki ijayo likizo ya jumla nchini Norway, inakwisha na watuwengi waliokuwa likizo wanarudi makazini. Watu wanashauriwa kuwa waangalifu kuepuka sehemu zenye kadamnasi ya watu wengi. Watu wawe makini inapohusu masuala ya afya.
No comments:
Post a Comment