Omer Bhatti:
”Mimi siyo mtoto wa Michael”
Omer Bhatti, 7. Julai mwili wa Michael ulipoagwa.
Kijana Omer Bhatti (miaka 25), kutoka Holmlia, Oslo amekanusha uvumi kuwa eti yeye ni mtoto wa Michael Jackson. Uvumi huo ulianza alipoonekana amekaa mbele pamoja na familia nzima ya marehemu Michael Jackson, siku mwili wa Michael ulipoagwa Julai 7. Amekanusha uvumi huo kwenye gazeti la Sunday Mirror ya Uingereza. Hivi karibuni vyombo kadhaa vya habari, haswa vya Uingereza vimekuwa vikidai kuwa, Omer ni mtoto wa Michael, kuwa Michael alipokuwa ziarani mjini Oslo, alitembea na mama Omer.
Amesema kuwa amekuwa karibu sana na Michael, kwa karibu miaka 10. Mwaka 1996 alizungumza duniani kwenye konseti za Michael na ameishi kwenye makazi ya Michael, Neverland.
No comments:
Post a Comment