Apple kuchunguza
kulipuka kwa iPhone
Kijana mmoja wa Kifaransa amepata jeraha baya la jicho, baada ya iPhone yake kumlipukia. Hayo yamesemwa na msemaji wa kitengo kinachoshughulikia usalama wa bidhaa cha kamishna ya nchi za Ulaya (EU Consumer Affairs).
Kampuni ya Apple inayomiliki iPhone imesema kuwa inachunguza tukio hilo lililotokea nchini Ufaransa na mengine yanayohusu simu hizo za aina ya iPhone na kuwa hawatotoa maelezo yoyote kwa sasa hadi uchunguzi wa matukio hayo utakapomalizika.
Chanzo: Reuters
No comments:
Post a Comment