Thursday, August 20, 2009

Caster Semenya apimwa

Jinsia yake.








Mkimbiaji wa kike wa mita 800 kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya (miaka 18) amepimwa jinsia yake na shirikisho la michezo ya riadhaa duniani (IAAF) na matokeo yanaonyesha kuwa Caster ni mwanamke. Kupimwa kwa Caster kumefanyika baada ya mwanariadha wa zamani wa Norway, Steinar Hoen kusema:

“Caster amekaa kidume dume, angalia alivyokaa kaa na jinsi anavyokimbia”.

Hoen alisema hayo alipokuwa akitoa maoni yake kwenye kituo cha luninga cha Norway, NRK kwenye uwanja wa Olimpiki, mjini Berlin. Msemo huo ulinaswa na vyombo vya habari na wapenda michezo ya riadha duniani na IAAF ikaamua kumpima Caster jinsia yake. Msemaji wa IAAF, Nick Davies alisema kwa kuomba samahani na kwa masikitiko, kwa nini walichukua hatua ya kumpima Caster.

Jana, Caster alinyakua medali ya dhahabu jana kwenye fainali za mbio za mita 800 kwa dakika 1:55:45

Bofya na angalia wasifu wa Caster Semenya.

No comments: