Atapeliwa kroner 30 000 London
Mwenyewe akiwa Oslo!
Wizi wa kadi za benki unaongezeka kila kukicha.
Kijana mmoja, Anders (20) wikiendi iliyopita ametapeliwa kr. 30 000 (Tshs. 6 586 460,-) toka kwenye akaunti yake kwenye Automatic Teller Machine (ATM) moja mjini London, huku mwenyewe akiwa Oslo!
Benki ya posta ndio waliompigia simu na kumwarifu kuwa wana wasiwasi kuwa ametapeliwa hela zake hivyo akatoe ripoti polisi. Benki ya posta wakafunga mara moja akaunti yake kwa tahadhari. Kijana huyo alipiga simu polisi, na walimwambia aende haraka akatoe taarifa za kuibiwa kwake. Alipofika kwenye kituo cha kati cha polisi mjini Oslo, polisi walimwambia kuwa si yeye peke yake. Watu wengi wiki hii wamechukuliwa hela kwenye akaunti zao nje ya nchi huku wenyewe wakiwa hapa hapa Norway.
Wengine wamegundua kuwa hela zao zimechukuliwa kwenye duka moja (Deli de Luca) maeneo ya Greenland (Grønland) mjini Oslo, wakati hawajawahi kukanyaga kwenye hilo duka.
Jeshi la polisi na mabenki wanatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na kuangalia akaunti zao mara kwa mara. Mteja akiona walakini kwenye akaunti yake anatakiwa kutoa taarifa haraka polisi na kwenye benki yake.
No comments:
Post a Comment