Thursday, August 20, 2009

Ban Kim-Moon

kumtema Asha Rose Migiro?



Dr. Asha Rose Migiro


Mwanadiplomasia na balozi wa Norway kwenye Umoja wa Mataifa, Bi. Mona Juul ameiandikia wizara ya mambo ya nchi za nje ya Norway, taarifa ya siri jinsi katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Kim-Moon alivyoshindwa kufanya kazi. Hayo yaliandikwa jana na gazeti la hapa la kila siku, Aftenposten kuwa Ban Kim-Moon hajui kufanya kazi, haelewani na wafanyakazi walio chini yake na ana hasira za mkizi. Kwenye taarifa hiyo, inaonyesha kuwa Ban Kim-Moon haelewani kabisa na msaidizi wake, Bi. Asha Rose Migiro na tetesi kuwa huenda Ba Kim Moon akamtema Bi. Migiro kama msaidizi wake.

Bofya na soma taarifa hiyo (iko kwa Kinorwejiani)


1 comment:

Mzee wa Taratibu said...

Hapa sasa imekua ni ubaguzi wa rangi tena.