Sunday, August 09, 2009

Collable' sio ishu kama una

nyenzo shost komaa!


Achana ma mambo ya kizamani hakuna mazoea katika mapenzi na la msingi unalopaswa kufahamu vita ni vita shost, kama ulikuwa hujui hujachelewa anza leo, boresha mazingira yako ya mapenzi na hiyo itamfanya mke mwenzio awe katika wakati mgumu.

Mana ukiwa muelewa sio ajabu mke mwenzio akakutumia wewe kama mfano na hapo ndipo utakapopata pointi za ushindi katika sebene lenu upo hapo bimkubwa!

Si hivyo tu pamoja na hayo yote yapo mambo muhimu ambayo unapaswa kuyatilia maanani ili uwe juu siku zote ikiwa utayapa nafasi mambo haya utakuwa uko juu siku zote.

1.Hakikisha unaelewa vizuri chakula anachopendelea mumeo, si hivyo tu jitahidi kuwa makini katika uandaaji wa chakula chake pale unapopata nafasi si unajua kwa sasa wanawake wengi wapo bize kusaka mahela, usijisahau sana katika hilo.

2.Mawasiliano ni muhimu sana hakikisha unamjulia hali kila mara ili kuweka mazingira ya kukumbuka muda wote, kwani kwa kufanya hivyo utaufanya ushusiano wenu uwe imara .

3.Kuwa makini katika shughuli za maendeleo, hakikisha matumizi yako yanakuwa ya kawaida, ukitilia mkazo masuala ya maendeleo ya familia yenu kama vile ujenzi wa nyumba n.k

4.Masuala ya ugomvi baina yenu yatatuliwe kabla ya usiku kukucha hii itawapa mwanga bora wa kusonga mbele.

5.Sheria muhimu za ndoa zitekeleze shost ujeuri hauna nafasi katika maisha hayo, ya vikiweni yaache kijiweni nyumbani kwako sio mwake

6.Boresha miundo mbinu dada usitafute mchawi wakati we mwenyewe unajiwangia!

7.Heshima kitu cha bure jiheshimu utaheshimiwa sin a mumeo bali hata na huyo mke mwenzio matusi si mahala pake shost!

8.Zawadi ni muhimu katika kucheza karata zako, usiwe hodari wa kupokea toa shoga ili ujiwekee nafasi nzuri ya kupata yaliyo mazuri kutoka kwa umpendaye.

Kwa leo naishia hapa shost wangu akili kumkichwa! Kumkimbia mwanamke mwenzio aibu dada hasa akikuta! Tuonane wiki ijayo

Na Shangazi mkubwa

Kutoka Mwananchi


No comments: