Sunday, August 09, 2009

”Obama” wa Urusi



Bango la kampeni ya uchaguzi la Crima

Joaquim Crima anajiita ”Volgograds Obama”. Miaka 37 ana asili ya Guinea Bissau. Amesoma Urusi na ameamua kuishi kwenye mji wa Srednyaya Akhtuba, mji wenyewakazi 55000, kusini ya Urusi. Crima alienda Urusi mwaka 1989 na amehitimu kama mwalimu toka chuo kikuu cha Volgograd. Ana shamba kubwa la hekari 200 na ameajiri wafanyakazi 20. Amejiunga na chama cha waziri mkuu Vladimir Putin. Na Oktoba mwaka huu, atagombea umeya wa Srednyaya Akhtuba. Lengo lake ni kufika kwenye ngazi za juu na ikiwezekana kuwa na ofisi Kremlin.


No comments: