Tuesday, August 04, 2009

Henry Joseph kacheza,

Kongsvinger 2 – Nybergsund 0



Henry Joseph Shindika mchezaji kiungo wa Kongsvinger.


Mchezaji wa soka wa zamani wa timu ya Simba ya Dar es Salaam na kapteni wa Taifa Stars, na ambaye sasa anachezea timu ya Kongsvinger, Henry Joseph hakupata nafasi ya kucheza tokea mwanzoni, wakati Kongsvinger ilipowafunga Nybergsund kwa magoli 2 – 0. Hivi sasa Kongsvinger iko kwenye nafasi ya tatu ya ligi ya Adecco (si ligi Kuu, ila ni ligi ya daraja la kwanza). Mechi hiyo ilionyeshwa ”live” na kituo cha luninga ya taifa, NRK 2. Goli la kwanza la Kongsvinger lilifungwa na Andreas Moen kwenye dakika ya 44 kabla ya mapumziko. Goli la pili lilifungwa na Kai Risholt kwenye dakika ya 70. Dakika ya 80 ya mchezo, Henry Joseph Shindika aliingia kuchukua nafasi ya Jonas Johansen. Henry ameonyesha kuwa kama akipewa nafasi, anaweza kufanya vizuri kwenye ligi ya Adecco. Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Kongsvinger uitwao Gjemselund.


No comments: