Henry Joseph kucheza leo
SHIRIKISHO la Soka la Norway (NFF = Norges Fotballforbund), limeiruhusu timu ya Kongsvinger kumtumia Henry Joseph katika mchezo wake wa leo Jumanne baada ya kupata kibali kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Leseni ya kwanza kuwasili ilikuwa ni ya beki, Yngvar Hakonsen aliyepata kibali chake Ijumaa wakati kibali cha Henry Joseph kilitua Jumamosi.
Mkurugenzi wa michezo wa Kongsvinger, Morten Kristiansen alithibitisha kupokea ITC za wachezaji hao. Henry na Hakonsen wataanza kucheza mechi yao ya kwanza leo Jumanne dhidi ya timu ya Nybergsund itakayoonyeshwa moja kwa moja na televisheni za Norway.
Henry Joseph atavaa jezi namba mbili wakati Yngvar Hakonsen atavaa jezi namba 15. Henry Joseph alisajiliwa na Kongsvinger akitokea Simba na ameingia mkataba wa miaka minne.
No comments:
Post a Comment