Thursday, August 06, 2009

Liverpool 2 – FC Lyn Oslo 0



Andrei Voronin mfungaji wa goli la kwanza akijaribu kumtoka Stanley Ihugba wa Lyn.


Glen Johnson wa Livepool kulia akikimbilia mpira na Erling Knudtzon wa Lyn.


Kama kawaida kabla ya ligi kuu ya Uingereza kuanza, timu ya Liverpool imefanya ziara ya mechi moja ya kirafiki na FC Lyn ya Oslo. Kabumbu limechezwa jana kwenye uwanja wa Bislet mjini Oslo. Lyn ambayo inashika mkia kwenye ligi kuu ya Norway (tippeligaen), iliwabana masupastaa wa Liverpool karibu dakika 43. Dakika ya 44, Liverpool walipata goli la kwanza lilifungwa na Andrij Voronin. Baada ya mapumziko, FC Lyn waliwabana sana Liverpool, lakini wakashindwa kutumia vizuri nafasi walizopata. Liverpool walifanya mabadiliko kadhaa: Damien Plessis aliingia badala ya Lucas, Javier Mascherano badala ya Spearing, Philip Degen badala ya Johnson, Alberto Riera badala ya Babel na Yossi Benayoun badala ya Kuyt. Dakika ya 59, David Ngog alifunga golila pili. Dakika ya 62, Liverpool walifanya mabadiliko tena. Waliwatoa Ngog, Andrej Vorovin, Dossena San Jose Dominguez na kuwaingia; Steven Gerrard, Fernando Torres, Emiliano Insua na Daniel Ayala. Lakini vijana wa FC Lyn walikataa kufungwa zaidi ya magoli mawili. Hii ni mara ya 22 kwa Liverpool kucheza mechi za kirafiki hapa Norway. Wameshinda 12, wametoka sare 4 na wamefungwa 5.

Timu zilikuwa hivi:

Lyn (fomesheni 4-4-2): Tyrel Lacey – Magne Simonsen, Mads Dahm, Vegar Gjermundstad, Shane Stefanutto – Endre Fotland Knudsen, Stanley Ihugba, Paul Obiefule, Erling Knudtzon – Davy Claude Angan, Jo Inge Berget
Marizevu: Arnar Darri Petursson, Jimmy Tamandi, Rikard Nilsson, Tommy Berntsen, Fredrik Dahm, Edwin Kjeldner, Nick Webb, Kim Holmen, Gøran van den Burgt

Liverpool (fomesheni 4-2-2): Diego Cavalieri - Glen Johnson, Mikel San Jose Dominguez, Martin Kelly, Andrea Dossena - Dirk Kuyt, Jay Spearing, Lucas Leiva, Ryan Babel - Andrij Voronin, David Ngog
Marizevu: Peter Gulasci, Damien Plessis, Philip Degen, Steven Gerrard, Fernando Torres, Albert Riera, Yossi Benayoun, Daniel Ayala, Javier Mascherano, Emiliano Insua, Jamie Carragher

Refa: Brage Sandmoen, Kjelsås

No comments: