Mkewe ambebesha bango,
baada ya kumfumania
Mwanaume mmoja nchini Marekani itambidi afikirie mara mbili mbili kutoka nje ya ndoa yake siku nyingine baada ya kupewa adhabu hii kali ya kufedhehesha. Alilazimika kukubali adhabu ya kufedhehesha baada ya mkewe kumnasa akiisaliti ndoa yao.
William Taylor alilazimishwa na mkewe kusimama kwenye maungano ya barabara kuu ya Tyson’s Corner karibu na kituo cha basi kwenye eneo ambalo liko bize sana nyakati za asubuhi na jioni mbele ya Tysons Corner Mall, Centreville, Virginia huku akiwa amebeba bango linalosema "Nilitembea nje ya ndoa na hii ndiyo adhabu yangu".
Adhabu hiyo ambayo ameanza kuitekeleza jana ili aweze kusamehewa, Taylor alisema kuwa ataendelea kusimama na bango hilo kwenye eneo hilo kwa wiki nzima.
Taylor alikuwa akiwaambia wapita njia kuwa mkewe aliamua kumpa adhabu hiyo baada ya kupata ushahidi wa kutosha kupitia simu yake kuwa alikuwa akiisaliti ndoa yao.
"Mwanzoni nilifikiri alikuwa akinitania, lakini alisisita kuwa lazima nifanye hivyo kama nataka kusamehewa" alisema Taylor akiongea na mtangazaji wa televisheni ya FOX 5.
"Niliona bora nifanye anavyotaka ili niweze kuikoa ndoa yangu, na ndiyo kama unavyoniona hapa" alisema Taylor.
Taylor huanza kusimama kwenye eneo hilo mida ya asubuhi kuanzia saa tatu na husimama hapo kwa masaa mawili.
Chanzo: Fox News
No comments:
Post a Comment