Kuelekea uchaguzi mkuu Norway:
Chama cha wahafidhina wenye
siasa kali (FrP) wakishinda
watakata misaada kwa
Tanzania na Uganda
Chama cha wahafidhina wenye siasa kali hapa Norway, Fremskrittspartiet (FrP)/the Progress Party, kimetoa ilani zake watakazotekeleza katika siku 100 ikiwa watashinda kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatatu, 14, Septemba, 2009 (Uchaguzi mkuu hufanyika Jumatatu ya pili ya Septemba kila baada ya miaka minne).
Wameahidi kuwa watakapoingia madarakani, watahakikisha wanaziba nyufa zote zilizopo kwenye sheria ya uhamiaji, ili kuwabana wageni wanaoingia isivyo halali kuomba ukimbizi huku wakiwa si wakimbizi wa kweli. Watahakikisha kuwa wote wale wataokuja kuomba ukumbizi wanawekwa kwenye kambi zenye ulinzi ili wasizurure mitaani bila mpango na pia watahakikisha kuwa kila fomu ya mwombaji wa hifadhi ya ukimbizi, inajibiwa baada ya masaa 48 na atayenyimwa hifadhi ya ukimbizi anaondolewa mara moja bila huruma.
Kwenye ilani ya mwisho (namba 3.4 ipo kwa Kinorwejiani) wanapendekeza kukata misaada kwa Tanzania na Uganda kwa kushindwa kutumia vizuri misaada inayotolewa na Norway miaka nenda, miaka rudi.
Bofya na usome ilani za Fremskrittspartiet (FrP) ziko kwenye PDF na kwenye lugha ya Kinorwejiani.
Bofya na usome ”A Change for the Future, A Brief Introduction to the Progress Party”
No comments:
Post a Comment