Sunday, August 23, 2009

Mtoto wangu ni mwanamke!

Asema mama wa Semenya.



Mama Caster, Bi. Dorkus Semenya


Caster Semenya.


Mama wa mkimbiaji wa mita 800 toka Afrika Kusini Dorkus Semenya, anasema watu waache kumwandama mtoto wake, Caster Semenya. Caster ni mwanamke. ”Mimi ndiye mama yake, nimemzaa na najua kuwa mtoto wangu ni mwanamke” anasema mama huyo.

Kumekuwa na tetesi, maneno na maoni tofauti juu ya jinsia ya Caster Semenya toka ashinde medali ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha ya dunia mjini Berlin. Afrika Kusini imekasirishwa sana na tuhuma zinazotolewa kuwa Caster ni mwanamme na kusema huo ni ubaguzi wa rangi.


No comments: