Tuesday, August 04, 2009


Mwanamke kortini kwa tuhuma

'kumuoa binti'




Na Burhan Yakub,Tanga

MWANAMKE mkazi wa jijini hapa, Aisha Mohamed jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga akikabiliwa na tuhuma za kumfanyia vitendo vya usagaji msichana mwenye miaka 20 na kumdhalilisha.

Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Tanga Ramla Shehagilo mwanasheria wa serikali Rebeca Mwangoso alidai mahakamani hapo jana kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 20 mwaka huu eneo ya Kwaminchi jijini Tanga kwa kumdhalilisha kijinsia msichana huyo (jina linahifadhiwa)

Wakili huyo alidai Mahakama hapo kuwa mshtakiwa huyo alikuwa na kawaida ya kumfanyia vitendo hivyo msichana huyo tangu mwaka 2008 na inadaiwa alikuwa akimhadaa kwa zawadi mbalimbali kama vile suruali za jinsi.

Mtuhumiwa huyo aliwasilisha barua ya kuomba dhamana na kiapo kutoka ofisi ya Upelelezi lakini mahakama hiyo ilitupilia mbali dhamana hiyo kutokana na usalama wa mtuhumiwa huyo akiwa uraiani

Kutoka Mwananchi

No comments: