Saturday, August 15, 2009

Ndege yaanguka ghafla shambani





Ndege ndogo aina ya Piper J-3 Cub jana kwenye saa 10 jioni ilianguka shambani kwenye kijiji cha Elvenes, maeneo ya Salangen (Norway). Rubani wa ndege hiyo, Ketil Løvhaug (haukuumia) alisema kuwa hajui kilichotokea alipokuwa angani. Alishtukia ndege inaanguka! Rubani huyo hakutaka kutoa maelezo zaidi. Amesema anaachia uchunguzi wa polisi na wa kamishna ya ajali.

Chanzo: Salangen Nyheter


No comments: