Pinda aomboleza vifo vya
wanafunzi 12 wa Idodi
WAZIRI Mkuu Mh. Mizengo Pinda ametoa salamu za rambirambi na pole kwawazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi 12 wa shule ya Sekondari ya Idodi mkoani Iringa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na ajali yamoto iliyotokea shuleni hapo usiku wa kuamkia leo (Jumapili Agosti 23,2009).
Katika salamu hizo, Waziri Mkuu amesema, kwa niaba ya Serikali nakwa niaba ya yeye mwenyewe binafsi, amesikitishwa na kuhuzunishwa sana natukio hilo na vifo hivyo na kuwaomba wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wamarehemu kuwa wavumilivu na wavute subira katika kipindi hiki kigumu chamajonzi.
Alitaka waliojeruhiwa katika tukio hilo watibiwe vizuri nao wapate ahueni haraka.
Chanzo cha moto huo hakijathibitishwa rasmi, lakini kuna habarikuwa huenda kikawa ni mshumaa uliowaka na kusahauliwa na mwanafunzialiyekuwa anajisomea usiku.
Katika tukio hilo la moto, wanafunzi 12 wamefariki dunia na 23wamejeruhiwa. Kati ya majeruhi hao, 14 walikimbizwa na kulazwa hospitaliIringa na wengine 9 walikuwa wakitibiwa katika kituo cha afya cha Idodi.
Maiti wamepelekwa hospitali Iringa kwa ajili ya kutambuliwa rasmikabla ya taratibu za mazishi.
Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi.
Amin.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAA
Jumapili, Agosti 23, 2009
No comments:
Post a Comment