Wanafunzi 12 wateketea
kwa moto
Habari LEO
Wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodi inayomilikiwa na serikali, iliyopo Tarafa ya Idodi, Iringa Vijijini mkoani Iringa, wamefariki na kuteketea kabisa kwa moto baada ya bweni walimokuwa wamelala kuangamizwa kwa moto.
Wanafunzi hao ambao ni wasichana, wamepoteza maisha usiku wa kuamkia jana baada ya chumba kimojawapo cha bweni la wasichana (Nyerere Hostel), kushika moto kisha bweni zima kuteketea…..bofya na endelea>>>>>
Mwananchi
WANAFUNZI 12 wa kike katika Shule ya Sekondari ya Idodi, wilayani Iringa, wamekufa kwa kuteketea kwa moto na wengine 23 wamejeruhiwa vibaya, katika tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana.
Habari za awali zilisema kufa na kujeruhiwa kwa wanafunzi hao, kumetokana na moto ulioteketeza kabisa bweni lao, saa 8:00 usiku wakati wakiwa wamelala…..bofya na endelea>>>>>
Tanzania Daima
WANAFUNZI wa kike 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodi, mkoani Iringa, wamefariki dunia na wengine zaidi ya 22 kujeruhiwa, baada ya kuunguzwa kwa moto ulioteketeza bweni lao la Nyerere House.
Tukio la kusikitisha, lilitokea usiku wa kuamkia jana, majira ya saa saba usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wamelala kwenye bweni hilo lenye vyumba 25 na uwezo wa kulaza wanafunzi 461….bofya na endelea>>>>>
Uhuru
WANAFUNZI 12 wa kike wa sekondari ya Idodi, wilayani Iringa Vijijini, wamekufa na wengine 23 kujeruhiwa baada ya bweni walilokuwa wamelala kuteketea moto.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla, alisema moto huo ulitokea saa nane usiku wa kuamkia jana, ambapo mali kadhaa za wanafunzi hao ziliteketea…..bofya na endelea>>>>
No comments:
Post a Comment