Friday, August 07, 2009

Wafainiwa kwa kufanya

mapenzi kanisani



Tolu Akintepe, 30, na mke wake Bunmi, 28:
"Tulikuwa tunaweka viungo kuongeza utamu wa mapenzi yetu"


Tolu Akintepe, 30, na mke wake Bunmi, 28, wametozwa faini ya paundi 100 baada ya kubambwa wakifanya mapenzi juu ya madhabahu au maarufu kama 'Meza ya bwana' (meza inayokuwa mbele kabisa kanisani).

Kwa mujibu wa The Daily Metro, wanandoa hao walibambwa na mchungaji wa kanisa hilo dogo la Pentekoste lililopo katika kitongoji cha Ikeja jijini Lagos.

Mchungaji Gbenga Akhiomu aliwataka wanandoa hao walipe fidia ya Paundi 100 kwa kuivunjia heshima madhabahu. Mchungaji huyo pia aliwataka wanandoa hao waisafishe madhabahu na kisha wasali kuomba msamaha.

Katika hali iliyowaacha watu wengi mahakamani wakibaki na kicheko, wanandoa hao walimwambia jaji Ifeanyinwa Okenwa kwamba walifanya kitendo hicho ili kuongeza viungo vya kuamsha mapenzi yao ambayo yalikuwa yameanza kufifia baada ya ndoa yao ya miaka minne.

"Mke wangu amekuwa akiniambia mara kwa mara kwamba anataka tuyakuze mapenzi yetu kwa kufanya kitu kisicho cha kawaida" alisema Akintepe.

"Nilifikiria kuwa litakuwa wazo zuri kama tutafanya mapenzi kanisani huku Mungu akituangalia. Nilijua ni wazo linalohitaji ujasiri. Nilimwambia mke wangu naye akalipenda sana".

Jaji Okenwa aliwaonya wanandoa hao waheshimu taasisi za dini na aliwaamuru walipe faini ya paundi 100.

Wanandoa hao waliridhika na hukumu hiyo na walijitolea kulisafisha kanisa zima kwa muda wa wiki moja
.

No comments: