Friday, August 07, 2009

Ufisadi si Tanzania tu..

ndege 4 za kivita, zauzwa kwa

dala 5 kila moja. Gharama halisi

Dala milioni 3.7



MiG-31. Inaitwa "Foxhound" na nchi za NATO.
Moja ya ndege za kivita zinaenda kasi duniani. Ikiwa kwenye
spidi ya juu ni Mach 3, ama mara tatu zaidi ya mlio wa sauti.


Moscow (na RIA Novosti): Waendesha mashtaka kwenye mkoa wa Nizhny Novgorod wamefungua kesi ya jinai, ya mauzo miili ya ndege 4 za kivita isivyo halali. Miili (fuselage) ya ndege hizo za aina ya MiG-31 ”Foxhound” iliuzwa kwa Dala 5 za Kimarekani kila moja, badala ya gaharama yake halisi ya Dala milioni 3.7 kila moja. Hayo yamejulikana baada ya tume ya kuchunguza rushwa, ilipofanya uchunguzi wa ghafla wa silaha kwenye kiwanda kinachotengeneza ndege za kivita; Sokol Aircraft Construction Plant kilichoko kwenye mji wa Volga, mkoa wa Nizhny Novgorod.

Kampuni mmoja ya kwenye ”briefcase” iitwayo Metalsnab ndiyo ilifanya manunuzi hayo kwa kushirikiana na ofisa mmoja fisadi wa ”Agency for State Reserve”. Kampuni hiyo haiusiki na ununuzi wa vifaa vya kivita. Waziri wa zamani wa ulinzi wa Urusi, Jenerali Pavel Grachev, ni mmoja wa viongozi wa ngazi za juu waliogundulika hivi karibuni kuhusika na ufisadi wa hali ya juu wa mauzo ya vifaa vya kivita.

Chanzo: RIA Novosti, Moscow, Urusi.

No comments: