Tuesday, September 08, 2009

Anusurika kupigwa na

Maustaadhi


Anti Asu

SHOGA anayetambulika kwa jina la Athumani maarufu ‘Anti Asu’mkazi wa jijini Dar es Salaam, amenusurika kutolewa roho kwa kipigo na watu walioonekana kuwa ni waumini wazuri wa dini ya Kiislamu baada ya kufanya mambo yaliyowaudhi maustadh hao wakati huu wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Agosti 31, mwaka huu, kwenye Kituo cha daladala cha Mikumi, kilichopo mbele ya Hoteli ya Travertine, Magomeni, Dar es Salaam ambapo dume hilo likitokea kusikojulikana liliibukia kituoni hapo kulikokuwa na watu kadhaa na kuanza kujifanya mwanamke.

“Ah, jamani leo n’tapigwa mwenzenu, bwana’angu nikimwambia nilikuwa nasasambua mpaka saa hizi sijui kama atakubali, mwenzenu n’taachika jamani,” alisikika akilalamika shoga huyo na kuwaudhi wanaume waliokuwepo kituoni hapo.

Kauli hiyo iliamsha hasira za wengi ambao walianza kumfuata huku wakimshambulia kwa maneno na lilipoona hatari inamkaribia likakimbilia kwenye basi moja lilokuwa limesimama na kutokomea.

Kutoka Global Publishers

No comments: